Na JPJ✍️✍️✍️
Kwanza ieleweke kwamba Muswada huu una mapendezo ya marekebisho ya Sheria tatu (3) ambazo ni:-
(i) Sheria ya Ajira na Uhusiano Kazini, Sura ya 366,
(ii) Sheria ya Taasisi za Kazi, Sura ya 300, na
(iii) Sheria ya Usimamizi wa Ajira za Wageni, Sura ya 436.
- EMPLOYMENT AND LABOUR RELATIONS ACT, (CAP 366):
- Kifungu cha 4 kinapendekezwa kurekebishwa ili kuboresha na kuongeza tafsiri ya baadhi ya misamiati iliyotumika katika Sheria.
- Kifungu cha 9 kinapendekezwa
kurekebishwa kwa kuongeza wigo wa tafsiri ya msamiati “senior management employee”. - Kifungu cha 14 kinapendekezwa kurekebishwa ili kubainisha aina ya mikataba ya muda maalum. Lengo la marekebisho haya ni kuongeza wigo
wa mazingira ambayo mtu anaweza kuajiriwa kwa mkataba wa kipindi
maalum, ikiwemo mikataba ambayo mwajiriwa anaajiriwa kwa muda ili
kuendana na ongezeko la wingi wa kazi, kutoa fursa kwa wahitimu wa
vyuo ili kuwajengea uwezo na kufanya kazi nyingine za misimu. - Kifungu cha 16A kinapendekezwa kuongezwa ili kubainisha mazingira ambayo mwajiri na mwajiriwa wanaweza kuingia katika makubaliano ya namna watakavyofanya kazi katika hali ya dharura inayoweza kuathiri uzalishaji mahali pa kazi.
- Kifungu cha 33 kinapendekezwa kurekebishwa ili kuongeza muda wa
likizo ya uzazi kwa mwajiriwa ambaye amejifungua mtoto njiti kwa kujumuisha katika likizo yake ya uzazi muda uliobaki kufikia wiki 36 za ujauzito. - Kifungu cha 34A kinapendekezwa kuongezwa ili kumwezesha mwajiri kumpatia mwajiriwa likizo bila malipo isiyozidi siku 30.
- Kifungu cha 37 kinapendekezwa kurekebishwa kwa kuweka masharti yanayozuia mwajiri kutoanzisha au kuendelea na shauri la nidhamu dhidi ya mwajiriwa pale
ambapo mgogoro huo upo mbele ya Tume au Mahakama ya Kazi. 👉Hii ina lengo la kuzuia uingiliaji wa mchakato wa ushughulikiaji
wa migogoro iliyowasilishwa kwenye Tume au Mahakama ya Kazi. - Kifungu cha 40 kinapendekezwa kurekebishwa ili kuainisha fidia kulingana na aina ya mgogoro na kuweka ukomo wa juu wa fidia inayotolewa kwa mwajiriwa aliyeachishwa kazi isivyo halali.
- Kifungu cha 41A
kinapendekezwa kuongezwa ili kuweka masharti kuhusu nafuu kwa uvunjaji wa mkataba wa ajira ya muda maalumu. - Kifungu cha 71 kinapendekezwa kurekebishwa ili kuweka masharti ya utaratibu wa kuanza kutumika kwa mikataba ya hali bora inayoingiwa na
wakuu wa taasisi za umma. - Kifungu cha 73 kinapendekezwa kurekebishwa ili kuwezesha vyama vya wafanyakazi kwa pamoja kuingia mikataba ya hali bora na mwajiri au vyama vya waajiri ya kuanzisha majukwaa ya ushiriki wa waajiriwa mahali pa kazi.
- Kifungu cha 86 kinapendekezwa kurekebishwa ili kuweka takwa la pande
zote katika shauri kuwepo wakati wa usuluhishi na kuzuia mwajiri kuwakilishwa na mwakilishi binafsi. Pia, 👉kifungu hiki kinapendekezwa kurekebishwa ili kuweka ukomo wa muda
wa kuwasilisha mgogoro kwa hatua ya uamuzi baada ya usuluhishi kushindikana. - Kifungu cha 87 kinapendekezwa
kurekebishwa ili kuzuia msuluhishi kuamua mgogoro uliopo katika hatua ya usuluhishi na badala yake kubainisha kwamba usuluhishi
umeshindikana. Pia, 👉kifungu kinapendekezwa kurekebishwa ili kuipa
mamlaka Tume (CMA) kurejesha shauri na kulisikiliza pale ambapo mwombaji
ametoa sababu za msingi za kutohudhuria awali katika usikilizwaji wa
mgogoro. - Kifungu cha 88 kinapendekezwa kurekebishwa ili kuweka masharti
kuhusu utaratibu wa utoaji wa tuzo ikiwa upande mmoja utakubali madai au sehemu ya madai, utaratibu wa kufanya maombi ya kutengua amri au uamuzi uliofanywa kwa kusikilizwa upande mmoja na wajibu wa mwamuzi kuwataarifu wahusika wa mgogoro endapo atashindwa kutoa
tuzo ndani ya siku 30. - Kifungu cha 94 kinapendekezwa kurekebishwa ili kuweka masharti ya kuzuia wahusika wa mgogoro kuwasilisha maombi ya mapitio kwa maamuzi madogo ya Tume isipokuwa kama maamuzi hayo yana athari ya
kumaliza mgogoro. - Kifungu cha 97 kinapendekezwa kurekebishwa ili kuweka utaratibu utakaowezesha
nyaraka za Tume kusambazwa na msambazaji nyaraka wa mahakama.