THE NON-CITIZENS (EMPLOYMENT REGULATION) ACT, (CAP. 436):
- Kifungu cha 9 kinapendekezwa kurekebishwa ili kuweka masharti ya kumtaka raia wa kigeni mwenye kibali cha kazi daraja A anayekusudia kujihusisha na kampuni nyingine anayomiliki hisa kupata idhini ya
Kamishna wa Kazi. - Kifungu cha 10 kinapendekezwa kurekebishwa kwa kuweka masharti ya kuzuia urejeshwaji wa ada ya maombi ya kibali cha kazi.
- Kifungu cha 12
kinapendekezwa kurekebishwa ili kuwawezesha wakimbizi wenye hadhi stahiki kuendelea kufanya kazi bila kubanwa na sharti la ukomo wa muda wa kibali cha kazi. Pia, 👉kifungu hiki kinarekebishwa ili maombi ya kuhuisha kibali cha kazi kuwasilishwa kwa Kamishna wa Kazi angalau
miezi miwili kabla ya kuisha kwa muda wa kibali.