- Kifungu cha 2 kinapendekezwa kurekebishwa ili kuboresha tafsiri za
baadhi ya misamiati iliyotumika katika Sheria. - Kifungu cha 9 kinapendekezwa kurekebishwa ili kubadili
utaratibu wa vikao vya Baraza kutoka katika utaratibu wa mwaka wa
kalenda na badala yake kutumia utaratibu wa mwaka wa fedha. - Kifungu cha 15 kinapendekezwa kurekebishwa ili kuweka masharti ya kumzuia msuluhishi aliyehusika katika usuluhishi wa mgogoro katika
ngazi ya usuluhushi kuamua katika ngazi ya uamuzi. - Kifungu cha 16
kinapendekezwa kurekebishwa ili kuweka masharti kwa Mwenyekiti
kuongoza vikao vya Tume na kama hatakuwepo, wajumbe waliopo
watateua mjumbe mmoja kuongoza kikao. - Kifungu cha 19 kinapendekezwa kurekebishwa ili kuondoa masharti
yanayoruhusu msuluhishi aliyehusika katika usuluhishi wa mgogoro kusikiliza mgogoro huo katika ngazi ya uamuzi. - Kifungu cha 20 kinapendekezwa
kurekebishwa ili kuwezesha Tume kumwita tena shahidi ambaye
ameshatoa ushahidi ili kumdadisi na kumtaka kutoa ushahidi zaidi. - Kifungu cha 27 kinapendekezwa kurekebishwa ili kurekebisha makosa ya kiuandishi.
- Vifungu vya 43 na 44 vinapendekezwa kurekebishwa kwa kuondoa cheo cha Naibu Kamishna wa Kazi na kutambua maafisa elimu
kazi waliopo chini ya Kamishna wa Kazi. - Kifungu cha 45 kinapendekezwa
kurekebishwa kwa kuboresha majukumu ya maafisa kazi na kuongeza majukumu ya maafisa elimu kazi. - Kifungu cha 45A kinapendekezwa kurekebishwa ili kuboresha
masharti kuhusu ufifilishaji wa makosa kwa kuweka matakwa ya fedha
zinazolipwa katika ufifilishaji kuwekwa katika Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali. - Kifungu cha 55
kinapendekezwa kurekebishwa ili kumpa mamlaka Jaji Mkuu kwa
kushauriana na Waziri kutengeneza kanuni za kusimamia mienendo ya
wawakilishi binafsi. - Kifungu cha 56 kinapendekezwa kurekebishwa ili kuzuia
mwajiri kuwakilishwa na mwakilishi binafsi.